peoplepill id: saed-kubenea
SK
Tanzania
10 views today
10 views this week
Saed Kubenea
Tanzanian politician

Saed Kubenea

The basics

Quick Facts

Intro
Tanzanian politician
Places
Work field
Gender
Male
The details (from wikipedia)

Biography


Saed Kubenea ni mbunge wa jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kupitiachama cha CHADEMA.

Jimbo la Ubungo ni moja ya majimbo yaliyomo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo kambi ya upinzani ilifanikiwa kuyatwaa kupitia uchaguzi huo wa mwaka 2015 na kuwezesha kubeba viti vingi vya udiwani na hatimaye kushinda viti vya umeya. Upinzani ulitwaa kiti cha umeya cha Manispaa ya Kinondoni na baadaye Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Baadaye Wilaya ya Kinondoni iligawanywa na kuzaliwa manispaa ya Ubungo ikafanya uchaguzi mpya wa meya. Kinondoni ikachukuliwa na CCM katika uchaguzi uliojaa visa na upinzani kupitia mgombea wa Chadema, Boniface Jacob, ikatwaa kiti cha Ubungo.

Kabenea naendelea kuwa mmiliki na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kitanzania Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inayochapisha magazeti ya MwanaHALISI, MwanaHALISI Online, MwanaHALISI Forum na MSETO.

Gazeti la MwanaHALISI lililozaliwa Mei 2006 lilianza kupata msukosuko na serikali mwaka 2008 lilipofungiwa kwa mara ya kwanza kwa siku 90 (miezi mitatu). Mara ya pili likaja kufungiwa Juni 2012 kwa kuandika habari ya kiuchunguzi iliyobainisha mtandao uliopanga na kutekeleza njama ya kumteka na kumtesa karibu ya kumuua, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka wakati huo kikiwa kimetangaza mgogoro wa kimaslahi na Serikali. Mara ya tatu MwanaHALISI likafungiwa na serikali Septemba 2017. Wakati adhabu ya miezi mitatu ilimalizika, adhabu zilizofuatia zilifutwa na Mahakama Kuu baada kukubali pingamizi zilizofunguliwa na HHPL. Hata hivyo, mara ya mwisho serikali imeendelea kuzuia kuchapishwa tena kwa gazeti hilo kwa kutotoa leseni.

Anafahamika sana kwa kutoa habari nyingi za msingi wa makatazo na machukio dhidi ya watu walio mafisadi katika serikali ya watu wa Tanzania. Ni mwandishi mwenye malumbano makubwa kabisa katika nchi ya Tanzania.

Tarehe 5 Januari 2008 alivamiwa ofisini mwake na kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamika (saedkubenea.blogsport.com) ikambidi apelekwe nchini India kwa matibabu.

Tazama pia

  • Wabunge wa Tanzania

Marejeo

  1. Hata hivyo Gazeti la Mseto lilifungwa na Serikali Agosti 11 mwaka 2016 kwa kipindi cha miezi 36 (miaka mitatu) kwa madai ya kuchapisha habari iliyoambatana na nyaraka za kughushi.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saed Kubenea kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
The contents of this page are sourced from Wikipedia article. The contents are available under the CC BY-SA 4.0 license.
Lists
Saed Kubenea is in following lists
comments so far.
Comments
From our partners
Sponsored
Credits
References and sources
Saed Kubenea
arrow-left arrow-right instagram whatsapp myspace quora soundcloud spotify tumblr vk website youtube pandora tunein iheart itunes