peoplepill id: perpetua
P
4 views today
5 views this week
Perpetua
Martyre africaine

Perpetua

The basics

Quick Facts

Intro
Martyre africaine
Gender
Female
Birth
Place of death
Carthage
The details (from wikipedia)

Biography

Perpetua (181 - 7 Machi 203) alikuwa mama kijana mjini Karthago wakati wa Dola la Roma alipouawa kama shahidi wa imani ya Kikristo.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na wengineo kati ya watakatifu wafiadini na sikukuu yake ni tarehe 7 Machi.

Perpetua anakumbukwa pamoja na mtumwa na rafiki yake Felista na wavulana wanne ambao aliuawa pamoja nao: Saturus, Revokatus, Saturninus na Sekondinus.

Maisha

Perpetua alikuwa binti wa familia tajiri.

Kwenye umri wa miaka 22 aliolewa akapata mtoto. Wakati ule alijiandaa kubatizwa pamoja na watumishi wake Felista na Revocatus na kijana mwingine aliyeitwa Saturninus. Walikamatwa pamoja na mwalimu wao Saturus katika wimbi la dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Kwanza Perpetua alifungwa ndani na kupewa nafasi ya kuachana na imani yake. Alipokataa alihukumiwa adhabu ya kifo pamoja na wenzake. Gerezani walipokea ubatizo.

Perpetua alibembelezwa sana na babaye Mpagani aachane na Ukristo na kuokoa uhai wake, lakini alikataa.

Pamoja na wenzake aliuawa katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori.

Heshima baada ya kifo

Heshima iliyotolewa mara kwa wafiadini hao ilienea haraka katika Kanisa lote.

Masalia ya Perpetua yalihamishwa mara kadhaa kutoka na matatizo ya kihistoria. Hatimaye yamehifadhiwa huko Vierzon (Ufaransa).

Matendo ya Perpetua na Felista

"Matendo ya Perpetua na Felista" ni maandishi ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu ambazo zinasimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.

Filamu

  • Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
  • Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.

Tazama pia

  • Watakatifu wa Agano la Kale
  • Orodha ya Watakatifu Wakristo
  • Orodha ya Watakatifu Wafransisko

Viungo vya nje

Christian cross.svgMakala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Perpetua Mtakatifu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
The contents of this page are sourced from Wikipedia article. The contents are available under the CC BY-SA 4.0 license.
Lists
Perpetua is in following lists
comments so far.
Comments
From our partners
Sponsored
Perpetua
arrow-left arrow-right instagram whatsapp myspace quora soundcloud spotify tumblr vk website youtube pandora tunein iheart itunes