peoplepill id: eukeri-wa-lyon
EWL
2 views today
2 views this week
Eukeri wa Lyon

Eukeri wa Lyon

The basics

Quick Facts

Gender
Male
Religion(s):
Birth
The details (from wikipedia)

Biography

Eukeri wa Lyon (380 hivi - 449 hivi) alikuwa askofu mkuu wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa).

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Novemba.

Maisha na maandishi

Kisha kufiwa mke wake Gallia, alitawa pamoja na wanae Veranius and Salonius katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honoratus juu ya kisiwa karibu na Antibes.

Baadaye alihamia kisiwa cha Lerona (sasa Sainte-Marguerite), akisoma na kujitesa kwa lengo la kujiunga na Mababu wa jangwani.

Kumbe Yohane Kasiano alifika huko Marseille na kuandika sehemu ya pili ya Collationes (namba 11-17) kwa heshima ya Eukeri na Honoratus.

Wakati huohuo Eukeri aliandika De laude Eremi ("Sifa ya Jangwa") kwa askofu Hilari wa Arles.

Pia aliandika Epistola paraenetica ad Valerianum cognatum, de contemptu mundi kuhusu kudharau ulimwengu.

Liber formularum spiritalis intelligentiae inatetea uhalali wa kufafanua kiroho Biblia.

Kati ya maandishi yake kuna pia Institutiones ad Salonium, barua na homilia kadhaa n.k.

Kutokana na sifa yake, alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi; kwa msingi huo hakika alihudhuria Mtaguso wa Orange (441) akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.

Hapo mwanae Veranius alishika nafasi yake, na mwanae mwingine, Salonius, akawa askofu wa Geneva.

Tazama pia

  • Watakatifu wa Agano la Kale
  • Orodha ya Watakatifu Wakristo
  • Orodha ya Watakatifu wa Afrika
  • Orodha ya Watakatifu Wafransisko
  • Mababu wa Kanisa

Tanbihi

Marejeo

  • Salvator Pricoco, 1965. Eucherii De Laude eremi (University of Catania) This edition establishes the best, most recent Latin text.
  • Bishop of Tours Gregory, Historia Francorum (The History of the Franks) (London, England: Penguin Books, Ltd., 1974).
  • Ford Mommaerts-Browne, "A Speculation", http://archiver.rootsweb.ancestry.com/th/read/GEN-ANCIENT/2004-03/1079586413.
  • Sidonius Apollinaris, The Letters of Sidonius (Oxford: Clarendon, 1915) (orig.), pp. clx-clxxxiii; List of Correspondents, Notes, V.ix.1.
  • K. Pollmann, "Poetry and Suffering: Metrical Paraphrases of Eucherius of Lyons’ Passio Acaunensium Martyrum," in Willemien Otten and Karla Pollmann (eds), Poetry and Exegesis in Premodern Latin Christianity: The Encounter between Classical and Christian Strategies of Interpretation (Leiden and Boston: Brill, 2007) (Supplements to Vigiliae Christianae, 87).

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eukeri wa Lyon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
The contents of this page are sourced from Wikipedia article. The contents are available under the CC BY-SA 4.0 license.
Lists
Eukeri wa Lyon is in following lists
comments so far.
Comments
From our partners
Sponsored
Credits
References and sources
Eukeri wa Lyon
arrow-left arrow-right instagram whatsapp myspace quora soundcloud spotify tumblr vk website youtube pandora tunein iheart itunes