Sara Msafiri Ally
Quick Facts
Biography
Sara Msafiri Ally ni mwanamke aliyepata nafasi tofautitofauti katika jamii na serikali ya Tanzania. Nafasi alizoweza kupata ni
- Ubunge wa viti maalumu kundi la vijana.
- Mkuu wa wilaya ya Hanang, mkoa wa Manyara.
- Mkuu wa wilaya ya Kigamboni
Uteuzi
Tarehe 5 Agosti 2010 Sara Msafiri Ally aliteuliwa kuwa Mbunge wa viti maalumu kundi la vijana.
Tarehe 27 Juni 2016 aliteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Hanang, mkoa wa Manyara.
Tarehe 29 Julai 2018 Sara Msafiri Ally aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kigamboni akichukua nafasi ya Shaibu Mgandila aliyepangiwa wilaya nyingine. Nafasi yake katika wilaya ya Hanang ilichukuliwa na Joseph Mkirikiti.
Tarehe 3 Agosti 2018 aliapishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Utendaji kazi
Sara Msafiri Ally aliagiza halmashauri ya wilaya ya Hanang kufanya tathmini upya juu ya mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Shule ya Secondari ya Balang'dalalu na Kanisa la Pentekoste katika kijiji cha Balang'dalalu. Akahitimisha kwa kuiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kufanya tathmini ya ujenzi na gharama za kanisa lililopo eneo la shule ili kumlipa fidia mchungaji wa kanisa ndani ya siku 20.
Sara Msafiri aliagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge wa Hanang kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mary Nagu Jumatano (7 Machi 2018) akimtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye, jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali.
Sara Msafiri alifunga mafunzo ya mgambo, tarafa ya Bassotu kwa kukagua gwaride wilayani Hanang.
Marejeo
- ↑ http://bongondiyohome.blogspot.com/2010/08/ vijana-saba-wapeta-ubunge-uvccm-yumo.html
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-13. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/news/magufuli%E2%80%99s-axe-strikes-again
- ↑ http://www.pressreader.com/tanzania/ mtanzania/20180729/281496457086846
- ↑ http://bongondiyohome.blogspot.com/2010/08/ vijana-saba-wapeta-ubunge-uvccm-yumo.html
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/news/magufuli%E2%80%99s-axe-strikes-again
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/news/magufuli%E2%80%99s-axe-strikes-again
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-13. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
- ↑ ttps://dashboard.eatv.tv/news/current-affairs/mkuu-wa-wilaya-amaliza-mgogoro-hanang
- ↑ http://bongo5.com/mbunge-wa-ccm-mary-nagu-akamatwa-na-polisi-kwa-amri-ya-dc-03-2018/