Patrick Francis Imanjama
Quick Facts
Biography
Patrick Francis Imanjama amezaliwa 12 Juni 1959 huko visiwani Zanzibar Tanzania. Baba yake alikuwa ni askari polisi visiwani Zanzibar. Patrick Francis Imanjama ni msanii mchoraji wa picha za Etching, Picha za rangi za maji na picha za vitabuni. Patrick amefanikiwa kutengeneza kazi nyingi na kufanya maonyesho mengi ndani na nje ya nchi.
Maisha yake ya awali
Patrick Francis Imanjama amezaliwa 12 Juni 1959 huko visiwani Zanzibar. Wakati huo baba yake alikuwa askari polisi visiwani Zanzibar. Baada ya Patrick Francis kumaliza shule ya msingi alivutiwa sana na kazi ya sanaa ya painting. Mwaka 1975 alijiunga na kozi ya painting kwenye taasisi ya kijerumani iitwayo Goethe jiji Dar es salaam Tanzania. Mwaka 1982 alijiunga na taasisi ya “The Dar Es Salaam Art & Craft Centre”. ambapo Mwalimu wake Christine Stormberg Steinberg alimfundisha Patrick Francis mbinu za kuchora picha za etching.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Patrick Francis Imanjama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |