Hellen Kijo Bisimba
Quick Facts
Biography
Hellen Kijo Bisimba (alizaliwa mkoani Kilimanjaro, 10 Oktoba 1954) alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Center - LHRC) kuanzia 1/7/1996 hadi 30/6/2018.
Elimu yake
Alisoma Shule ya wasichana Weruweru [Kilimanjaro] Sekondari ya Awali 'o' Level na kumaliza Sekondari ya juu 'A' level Korogwe High School Tanga.Ana watoto wanne.
Dkt. Helen Kijo Bisimba amesoma shahada ya uzamivu ya sheria katika chuo kikuu (daktari wa falsafa) Warwick Uingereza 2008hadi 2011. Mnamo waka 2008 Dkt. Helen alipata tuzoakitambuliwa na ubalozi wa marekani nchini Tanzania kama ni mwanamke jasiriwa kwanza nchini Tanzania kwakupigania haki za binadamu baada ya kusimama na kutoa tamko dhidi ya serikali juu ya mauaji yaliyofanyika visiwani Zanzibar kwa waandamanaji yaliyotokea mwaka 2001.
Kazi
Amefanya kazi katika shirikia la LHRC kwa muda wa miaka 22 akiwa mkurugenzi mtendaji katika shirika hilo.
Dhamira yake ya kupigania na kuhamasisha haki za binadamu ilianza miaka ya sabini akiwa bado mwanafunzi wa sekondari kidato cha tano na sita mkoa wa Tanga, hii ni mara baada ya kugoma kuandika barua ya maelezo kwa mkuu wa shule iliyopelekea kusimamishwa masomo yake kwa muda.
Kitendo hiki kilimfanya awe mstari wa mbele kupigania haki za binaadamu kwa miaka takribani arobaini sasa.
Dkt.Helen Kijo Bisimba amestaafu kazi tangu Julai 2018.
Tanbihi
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hellen Kijo Bisimba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |