Blandina Changula
Quick Facts
Biography
Blandina Changula (amezaliwa tar. 27 Julai 1983 mkoani Shinyanga, Tanzania ni muigizaji wa vipindi vya telesheni na filamu nchini Tanzania.
Maisha ya Mwanzo
Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungoshule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.
Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi wa uigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi (Mr Ray), Tea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group. KwahivisasaBlandinaChagulakwakushirikiana namsaniimwenzakeVincentKigosiwanakampuniyaopamojaiitwayoRJ Company(Ray & Joharicoumpany ) ambayoinafanyakaziyakuzalishafilamumbalimbali kama vileBed Rest, Bad Luck , Wrong hope , Peace of mind , Fair Decision nk.
Baadhi ya Filamu Alizoigiza
- Sikitiko Langu
- Johari 1 na 2
- Dangerous Desire
- Dar 2 Lagos
Anaoshirikiana Nao
- Steven Kanumba
- Vincent Kigosi
- Muhsein Awadh
- Ally Chaowa
- Kulwa Kikumba
- Mwanaidi Suka
- Nuru Nassoro
- Ndumbagwe Misayo
- Donah Redson
- Fatuma Makongoro
- Emmanuel Myamba
- Charles Magari
- Fatuma Mvura
- Mohamed Mwikongi
- Fadhili Omar
Wanigeria
- Mercy Johson
- Nkilu Sylvanus
- Nancy Okeke
- Bimbo Ankintola
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Blandina Changula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |