Biography
Lists
Also Viewed
The basics
Quick Facts
Gender |
|
The details
Biography
Sesili wa Karthago (jina lake kamili kwa Kilatini lilikuwa Caecilianus) alikuwa padri wa mji huo (katika eneo la Tunisia ya leo) katika karne ya 3.
Mtu mwadilifu, ni maarufu hasa kwa kumsaidia Sipriani kuongokea Ukristo (245).
Kabla hajafa, Sesili alimkabidhi Sipriani kazi ya kutunza mke na watoto wake.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Juni.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
- ↑ Taz. "Vita Sancti Cypriani" kilichoandikwa na shemasi Ponsyo; Jeromu kimakosa alimuita Caecilius tu (De viris illustribus, 67, PL, XXIII, 714), na jina hilo fupi limezoeleka
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ https://catholicsaints.info/saint-caecilius-of-carthage/